The House of Favourite Newspapers

Faiza: Sugu Bado Ananipenda, Aweke Pesa Kwenye Akaunti – Video

MSANII wa Bongo Movie na mtangazaji, Faiza Ally amesema baba wa mtoto wake ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ bado anampenda na kudai ndiyo maana amekuwa hatimizi vyema majukumu yake kama baba kwa mtoto wao hivyo kumfanya Faiza kumsema mpenzi wake huyo wa zamani.

 

Faiza amefunguka hayo jana wakati akipiga Stori na Global TV Online kwenye ‘sherehe ya 40’ ya mtoto wa Zamaradi Mketema, King Salah iliyofanyika Bunju B jijini Dar es Salaam na kufunguka mengi ikiwemo utayari wa kurudiana na Sugu iwapo atarudi walee mtoto wao.

 

“Nadhani Sugu bado ananipenda ndiyo maana hatimizi vizuri wajibu wake wa malezi na matumizi kwa mtoto wake Sasha. Huenda anafurahi mimi ninavyokuwa ninamsema na mimi siwezi kuchoka kumsema mpaka pale atakapoweza kutimiza majukumu yake ipasavyo.

 

“Kama huhitaji kuwa na ishu na mtu basi unaweza kufanya mambo kwenye right way (njia sahihi), lakini ukiona mtu anakutafutia vitu vya kukuumiza ujue bado uko kwenye moyo wake, aweke pesa ya matumizi ya mtoto kwenye akaunti kila mwezi, atimize majukumu yake then ataona kama mimi nitaendelea kumfutalia,” alisema Faiza.

VIDEO: MSIKIE FAIZA AALY AKIFUNGUKA

Comments are closed.