The House of Favourite Newspapers

Kufuru: Diamond Amwaga Noti za Dola kwa Mtoto wa Zamaradi – Video

KINARA wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platinums amefanya kufuru ya aina yake baada kumwaga minoti ya dola akimzawadia mtoto wa mtangazaji Zamaradi Mketema, King Salah ambaye jana alifanyiwa sherehe ya 40 yake ya kuzaliwa.

Mkurugenzi huyo wa WCB alikuwa ameambatana na meneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’, msanii wake, Harmonize na mpenzi wake Muitaliano, Sarah ambaye pia alimzawadia Zamaradi mkwanja wa kutosha katika sherehe hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Zamaradi maeneo ya Bunju B, jijini Dar es Salaam.

 

VIDEO: SHUHUDIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.