The House of Favourite Newspapers

Familia ya Diamond Yawapa Tano Zari, Wema… Mama Mobeto Atokwa Povu!

FAMILIA ya Staa wa bongo fleva, Diamond Platinumz imewa imewamwagia misifa kwa kuwachambua waliowahi kuwa wapenzi wa kijana wao huyo ambapo imemtaja Zari The Boss Lady kama mwanamke msafi anayejua kutimiza wajibu wake kwa mwanamke, huku Wema akitajwa kuwa mwanamke anayejua kupika vizuri.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mama Diamond amebainisha sifa kuu ya Zari kuwa msafi huku mwanaye, Esma akikoment na kusema Wema ni mtaalam wa mapishi.

Baada ya maneno hayo, Mama Mobeto naye aliibuka na kutoa povu lake huku akisihi mwanaye kuwa mvumilivu hasa katika wakati huu mgumu kwake.

Kwa upande wake, Wema amemsifu Diamond kwa kuachia ngoma mpya ya Iyena aliyomshirikisha Rayvanny ambayo ndani yake yumo Zari na mpenzi wa Rayvanny, Fayvanny.

WEMA Atuma Ujumbe Mzito kwa Diamond, Baada ya Nyimbo ya Iyena

Comments are closed.