The House of Favourite Newspapers

Fei Toto Amchomoa Tshishimbi Yanga

KIUNGO mpya wa timu ya Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameibuka na kuweka bayana kuwa anatamani kupangwa eneo la kiungo mkabaji ndani ya timu hiyo nafasi ambayo imekuwa ikichezwa na kiungo Papy Kabamba Tshishimbi raia wa DR Congo.

Fei Toto ametua hivi karibuni katika kikosi hicho cha Yanga kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya Singida United kuridhia kumuachia kiungo huyo licha ya kumsajili kwa mkataba wa awali akitokea JKU ya Zanzibar.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Fei Toto ambaye pia anamudu kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji amesema kuwa kwake yupo tayari kwa ajili ya kupambania namba na mchezaji huyo kwenye eneo la katikati la timu hiyo katika msimu ujao wa ligi ambao utaanza Agosti 22, mwaka huu.

 

“Kwangu kokote pale nikipangwa ninacheza kati ya kiungo mchezeshaji au mkabaji lakini nikipangwa mkabaji itakuwa vizuri zaidi. Nimejiandaa kupambania namba na mchezaji yoyote yule na wala sina uoga juu ya hilo.

 

“Kambi yetu ya Morogoro ipo vizuri na wachezaji tunafurahia juu ya mazoezi ambayo tunapewa na makocha wetu, ninaamini tutakuwa fi ti kwa ajili ya kupambana na timu nyingine katika msimu ujao,” alisema Fei.

Said Ally, Dar es Salaam

Comments are closed.