The House of Favourite Newspapers

FERGUSON AWAPA UBINGWA LIVER

KOCHA wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson, amesema kuwa Liverpool watatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu. Ferguson amesema vita kubwa ya ubingwa ni kati ya City na Liverpool lakini yeye anaamini kuwa Liverpool ndiyo wenye nafasi ya ubingwa huo.

 

Amesema kuwa klabu itakayowazuia City kuchukua ubingwa ni Manchester United ambayo wamebakiza nayo amesema kama siyo kushinda basi United wanaweza kulazimisha sare kwenye mchezo ambao watacheza na City, Aprili 24.

 

Liverpool kwa sasa wapo kileleni wakiwa na pointi 85 zikiwa ni mbili mbele ya Manchester City wenye pointi 83, lakini wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

 

“Liverpool watachukua ubingwa msimu huu, naona kabisa wana nafasi hiyo kubwa kwa kuwa City bado wana mchezo na Manchester United. “Najua kama haitakuwa sare kwenye mchezo huo basi United wana nafasi kubwa ya kupata ushindi,” alisema Ferguson.

Comments are closed.