The House of Favourite Newspapers

Fid Q ageukia udairekta

0
fid qFarid Kubanda ‘Fid Q’,
Omary Mdose, Dar ess Salaam
MWANAMUZIKI wa Hip Hop Bongo, Farid Kubanda ‘Fid Q’, ameibuka na kusema kutokana na kushiriki kwa kiasi kikubwa kuandaa video mbili za wasanii hapa Bongo, muda si mrefu watu watakuja kufahamu uzuri wake kwenye udairekta. Fid Q, ambaye kwa sasa anatesa na Ngoma ya Walk It Of aliyomshirikisha Taz kuna kipindi fulani alikuwa kimya kwenye gemu jambo lililowafanya baadhi ya mashabiki wake kuhoji.

“Bado nipo najishughulisha na mambo ya muziki, na watu wanatakiwa kufahamu kwamba mbali na kuimba, pia mimi ni mkali wa ‘kudairekti’ video na tayari mpaka sasa nimefanya hivyo kwenye video mbili.
“Ya kwanza ni Walk It Of (aliyoimba mwenyewe), pia ya Ben Pol inayoitwa Moyo Mashine, natarajia kutengeneza zingine ili Wabongo wafahamu ninachofanya zaidi ya kuimba, kikubwa nashukuru video hii ya Ben Pol kupokelewa vizuri,” alisema Fid Q.
Leave A Reply