The House of Favourite Newspapers

First Eleven Yanga Usipime

Feisal Salum ‘Fei Toto’.

KOCHA wa Yanga,Mwinyi Zahera amewatamkia mashabiki wa klabu hiyo, habari nzuri ya kufurahisha ambayo imetokana na kazi pevu anayoifanya kambini mkoani Morogoro.

 

Mechi kubwa ya Yanga inayofuata ni Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Algers ya nchini Algeria itakayofanyika Agosti 19 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambayo ni ya kukamilisha ratiba kwani maji yameshazidi unga.

“Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu ya kujiandaa na ligi kuu lakini pia mechi yetu Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger ambayo tutacheza hivi karibuni. “Hali ya kikosi changu kusema kweli ni nzuri na ninavutiwa zaidi na hali ya kujituma uwanjani inayoonyeshwa kila siku na wachezaji wangu,” alisema Zahera ambaye ana uraia wa DR Congo na Ufaransa.

 

“Kuhusiana na kikosi cha kwanza kitakachokuwa kikianza katika michuano ya ligi kuu, tayari nimekipata lakini hakutakuwa na mchezaji ambaye atakuwa na uhakika wa namba kwa asilimia mia moja, mchezaji atakayekuwa akifanya vizuri mazoezini huyo ndiye atakayekuwa na nafasi kubwa ya kucheza,” alisema Zahera.

 

Licha ya kutotaja wazi majina ya kikosi hicho, lakini kulingana na mazoezi ambayo wamefanya inaonekana wazi kuwa golini atakaa kipa Klaus Kindoki, atasaidiana na walinzi Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vicent ‘Dante’, Kelvin Yondani viungo ni Papy Kabamba Tshishimbi, Rafael Daud, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Deus Kaseke na Mrisho Ngassa huku mbele akisimama mshambuliaji mmoja ambaye ni Heritier Makambo.

HABARI NA SWEETBERT LUKONGE

Comments are closed.