The House of Favourite Newspapers

Foden Ajitia Kitanzi Man City, Bosi Amtabiria Kuwa Mchezaji Bora Duniani

0
Phil Foden

KINDA wa Manchester City raia wa Uingereza Phil Foden ameongeza mkataba mpya klabuni hapo wa miaka mitano (5) unaotarajiwa kumuweka Etihad hadi majira ya kiangazi yam waka 2027.

 

Foden amekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu msimu huu hadi sasa akiwa tayari na jumla ya mabao 7 na pasi 3 za mabao ikiwa ni pamoja na Hat Trick yake aliyoifunga dhidi ya watani wake wa jadi Manchester United.

Foden ameongeza mkataba mpya wa miaka mitano

Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Txiki Begiristain amenukuliwa akisema kuwa Foden atakuwa moja ya wachezaji bora duniani kwa kipindi cha miaka michache ijayo.

 

“Tunajivunia kwa kile ambacho Phil amekipata hadi sasa, tunajua kuwa mambo mazuri bado yanakuja.

 

“Baada ya kusaini mkataba mpya sasa anatakiwa kuwekeza akili zake zote kwenye kufanya kazi na kuwa mchezaji bora duniani jambo ambalo tunaamini litakuwa.” amesema Begiristain.

 

Foden (22) amekuwa moja kati ya wachezaji tegemeo chini ya kikosi cha Kocha Pep Guardiola ambaye timu yake hadi sasa haijapoteza mchezo hata mmoja katika mbio za kuwania kikombe cha Ligi Kuu ya Nchini Uingereza EPL.

Leave A Reply