The House of Favourite Newspapers

Full Dozi Concert… Dully, Q Chillah Kutikisa Dar Live

0
Dully Sykes.

ULWAKONGWE wawili wasioshikika kunako gemu ya Bongo Fleva, Dully Sykes pamoja na Q Chillah wanatarajiwa kuungana na wakali wengine kibao katika Tamasha la Full Dozi litakalofanyika Jumamosi hii (Septemba, 9) ndani ya Uwanja wa Kima-taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Risasi Vibes, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema Full Dozi ni tamasha lililowaunganisha wasanii wa Muziki wa Dansi pamoja na Bongo Fleva huku akiwataka mashabiki na wadau wote wa burudani kujitokeza kwa wingi.

“Mbali ya Q Chillah na Dully tutakuwa na mkongwe, Juma Nature, Beka Flavour, Sholo Mwamba na Snura wakati upande wa Muziki wa Dansi itakuwepo bendi kongwe ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ikiongozwa na Luiza Mbutu,” alisema Mbizo.

Kiing-ilio katika tamasha hilo kitakuwa kiduchu yaani buku tano (5,000) tu getini.

Leave A Reply