The House of Favourite Newspapers

Full Time: Yanga 4-0 JKT Ruvu

yanga2

DAKIKA 90 za mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kati ya Dar es Salaam Young Africans ‘Yanga’ na JKT Ruvu huku Yanga wakiibuka vifua mbele baada ya kuwachabanga maafande wa JKT Ruvu bao 4-0.

Goli la kwanza la Yanga limeingizwa langoni na Obrey Chirwa kunako dakika ya 6 kwa shuti kali baada ya beki wa JKT Ruvu kuanguka na kuuacha mpira nyuma, Msuva akauwahi na kumpa Chirwa ambaye alimalizia kazi.

Amis Tambwe akitokea nje kwa kuchukua nafasi ya Donald Ngoma, dakika ya 61 anafunga bao la pili akiwa ametulia baada ya mabeki wa JKT kumsahau.

Dakika ya 83, Msuva anapachika bao la 3 baada ya kuunganisha pasi nzuri ya Tambwe huku dakika ya 90 Tambwe anapigilia msumali wa nne baada kuwavizia kipa na beki wa JKT Ruvu waliokuwa wamejisahau.

Comments are closed.