The House of Favourite Newspapers

G Nako Kahamia Muziki wa Injili? Ukweli Huu Hapa

0

 

MSANII wa Hip Hop kutoka Kampuni ya Weusi, George Mndeme ‘G Nako’ anayetamba na kibao chake kipya cha Lucky Me, amekanusha taarifa za yeye kuacha mziki wa Hip Hop na kuhamia kwenye muziki wa Injili.

 

Stori za yeye kuhamia kwenye muziki wa Injili zimeibuka hivi karibuni baada ya kuonekana akifanya shoo uwanja wa taifa katika tamasha la kidini ya kikristo huku video ya wimbo huo ikileta utata mkubwa kwa mashabiki zake na kuona kwamba mchizi amehamia katika kuimba nyimbo za dini.

 

 

Kitu kingine kilichowashangaza wengi ni baadhi ya vipande vilivyopo kwenye video hiyo ambayo inamuonyesha akiwa kwenye jeneza, kitu ambacho kimepelekea mashabiki kusema kuwa G Nako ni kama anakiona kifo chake siku za usoni.

 

“Kuimba wimbo wa dini si vibaya na haimaanishi kwamba nimeacha Muziki wa Hip Hop na kuhamia kwenye nyimbo za dini. Hata suala la kuonekana kwenye jeneza ni jambo la kawaida sana kwani hata waigizaji wa Marekani na sehemu nyingine wanaigiza.

 

 

“Niwaambie tu mashabiki zangu kwamba G Nako anabaki kuwa G Nako na wala wasishtuke kuniona nikiwa kwenye wimbo wenye mahadhi ya kidini wajue nimehamia huko,” alisema G Nako.

 

Mahojiano yake yote unaweza kuyaangalia kupitia chaneli yako ya kijanja ya Global TV Online iliyopo Youtube.

 

Stori: Isri Mohamed

 

Stamina, Darassa Kulipeleka Jiji Dar Live Sikukuu ya Idd Mosi

Leave A Reply