The House of Favourite Newspapers

Gabo Zigamba ‘Mgonjwa’ Wa Vitabu

0

MKALI wao huko Bongo Muvi, Salim Ahmed almaarufu kama Gabo Zigamba, amefunguka kuwa, yeye ni mtu anayependa sana kusoma vitabu kuliko hata kufanya starehe nyingine yoyote.

 

Akizungumza na Gazeti la Risasi Jumamosi, Gabo amesema kuwa anapenda kusoma sana vitabu vya Shaaban Robert, kwa wiki anaweza akaenda maktaba hata mara mbili au tatu.

 

“Sehemu yangu pendwa sana ninayopenda kwenda kutuliza akili ni Maktaba ya Taifa, pale ndipo utanikuta nasoma sana vitabu vya Shaaban Robert, lakini sio katika kumbi za starehe, huwa sina mambo hayo.

 

Kwa wiki naweza kwenda mara mbili au tatu.“Kwanza ni skills kuwa poa, la pili kuendelea kusoma kadiri unavyozidi kuishi, kwa hiyo mimi nimekuwa nikisoma vitabu mbalimbali hii inanifanya kuandika mambo yanayoeleweka mtandaoni,” alisema Gabo.

STORI: KHADIJA BAKARI

Leave A Reply