The House of Favourite Newspapers

Gamondi Aisuka Pacha Ya Straika Mpya Yanga

0

 

KATIKA kuhakikisha mshambuliaji wake mpya, Joseph Guede anapachika mabao, Kocha Mkuu wa Yanga, Muargentina, Miguel Gamondi ameanza kutengeneza kombinesheni nzuri ya viungo watakaomtengenezea nafasi nyingi za kufunga nyota huyo mpya.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu, nyota huyo atambulishwe na timu hiyo, mara baada ya usajili wake kukamilika katika dirisha hili dogo lililofungwa Januari, mwaka huu.

Straika huyo amesajili na Yanga akichukua nafasi ya Hafidh Konkoni aliyepelekwa kwa mkopo nchini Cyprus, baada ya kushindwa kumshawishi kocha Gamondi.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, kutoka katika benchi la ufundi ameliambia Championi Jumamosi kuwa kocha huyo ameanza kumpa mbinu za kufunga mabao katika kiwanja cha mazoezi.

Bosi huyo alisema kuwa kwa siku mbili ambazo mshambuliaji huyo amefanya mazoezi ya pamoja na timu hiyo, kocha huyo ameonekana akichezeshwa namba tisa huku nyuma yake wakiwepo Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli, Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ na Mudathir Yahya ambao wamekuwa wakibadilishana.

“Guede inavyoonekana alikuwa akifanya mazoezi ya kutosha kabla ya kusajiliwa, ni baada ya kuonekana ana fitinesi ya kutosha tofauti na wachezaji wengine waliosajiliwa na kupewa muda.

“Kocha ameliona hilo na kumpongeza, hivyo upo uwezakano mkubwa wa kuingia haraka katika kikosi cha kwanza, kikubwa anachotakiwa ni kuzoea ushindani wa lligi mapema.

“Tayari kocha ameanza kutengeneza muunganiko wake na viungo washambuliaji na wachezeshaji, kwa lengo la kuzoeana kwa haraka ili watengeneza kombinesheni nzuri itakayofunga mabao,” alisema bosi huyo.

Gamondi alimzungumzia mshambuliaji huyo kwa kusema: “Kila mchezaji mpya atakayekuja Yanga, ngumu kuingia katika kikosi cha kwanza moja kwa moja, hivyo atatakiwa kupata muda wa kuizoea ligi, pamoja na mifumo ya uchezaji wakiwemo hawa wachezaji wapya ambao tumewasajili dirisha dogo.”

STORI NA WILBERT MOLANDI

#EXCLUSIVE: MKE wa PROFESA JANABI -AFICHUA RATIBA ya KULA-ANAVYOWASAIDI WENYE SHIDA ya AFYA ya AKILI

Leave A Reply