The House of Favourite Newspapers

GDSS Wafanya Tathmini 2020

0
Ofisa Program Idara ya Habari na Mawasiliano, Jackson Malangalila akitoa somo.

Kupitia semina za jinsia na maendeleo (GDSS) ambazo zinaandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) imefanya tathimini ya mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwa kipindi cha mwaka mzima tangu Januari, 2020 hadi Desemba, 2020 na kuona namna jamii ilivyopata mafunzo.

Akizungumza kwenye Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) zinazoandaliwa na (TGNP), Ofisa Program Idara ya Habari na Mawasiliano, Jackson Malangalila amesema kuwa, wamefanya tathmini ya kile walichojifunza kwa mwaka mzima na kuitaka jamii kueleza kile ambacho wamekielewa kutoka kwenye semina hizo.

“Leo (jana jumatano) ni semina ya mwisho wa mwaka ambayo ni muhimu sana kwa jamii ambayo huwa inahudhuria ili kujadili mada ambazo wamejifunza, hivyo basi kila mwanajamii ameeleza kile ambacho amejifunza ni jinsi gani kimeweza kumpa msaada.

Mwanasemina akitaka ufafanuzi wa jambo.

“Wameeleza  masuala mbalimbali ikiwemo elimu na uwezeshwaji kiuchumi kwa makundi mbalimbali kama wanawake na vijana kupitia semina za jinsia na maendeleo (GDSS) katika mpango-mikakati wa kutokomeza ukatili katika jamii, uwepo wa bajeti ya kutosha endapo mhanga anapopata tatizo iwe rahisi kuchukuliwa na kufikishwa sehemu husika na kupata huduma kwa haraka.

“Wanajamii pia wameeleza namna ya uelewa wa sheria na mwenendo wa kesi za ukatili wa kijinsia zilivyo hivyo wametoa maoni yao kwamba kila mwanajamii akiona tukio la unyanyasaji wa kijinsia, anatakiwa atoe taarifa mapema ili ushahidi upatikane kesi iweze kufikia mwisho mapema.

“Aidha wameeleza kuwa wanawake wengi wamejitokeza katika kugombea kwenye nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu ulifanyika mwaka huu, kwa hiyo ni wazi kwa sasa wanawake wanasimama imara bila kuogopa katika mapambano ya aina yoyote,” alisema Jackson.

Mama huyu akiwa mbele ya wenzake kueleza yaliyomuingia katika semina hiyo.

Naye mmoja wa wadau wa semina hizo, Esta James aliiomba Serikali iongeze bidii katika kupambana na ukatili wa kijinsia na endapo mtu anayepatika na kosa hilo achukuliwe hatua kali ili wengine wasiendelee na vitendo hivyo.

“Ninaiomba Serikali iongeze juhudi za kupambana na ukatili wa kijinsia kama kubaka na kulawiti na suala zima la ukeketaji, yote yamefanikiwa kwa sababu sasa hivi huwezi kumkuta ngariba anamkeketa mtoto hadharani kwa kuwa anajua kama sheria itachukua mkono wake,” alisema Esta.

Leave A Reply