The House of Favourite Newspapers

GGML Yakabidhi Jengo Jipya la Ofisi kwa Kamanda wa Polisi Geita

0

Katikajitihada za kuboresha mazingira bora ya kufanyia kazi kwa taasisi mbalimbali zaSerikali, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imekabidhi jengo jipyakwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za jeshi la Polisi Mkoani Geita.

 

Akizungumzia ufadhili wa ujenzi wa jengo hilolenye ofisi tatu juzi mkoani Geita, Makamu wa Rais wa GGML anayeshughulikia miradi endelevu, Simon Shayo amesema kuwa pamoja na ukweli kuwa wanafadhili miradi mbalimbali yamaendeleo Mkoani Geita na Tanzania kwa ujumla, usalama wa miradi hiyo bado nijambo la msingi ambalo muda wote limekuwa likisimamiwa na jeshi la Polisi.

 

“Jeshila Polisi ni wadau wetu muhimu katika shughuli mbalimbali tunazozifanya. Tunashirikiananao katika maeneo mengi, hususani ulinzi mgodini na ulinzi shirikishi kwenyemitaa na vijiji vinavyotuzunguka.

 

“Tulipoonauhitaji wa ofisi kama mojawapo ya vikwazo vya utekelezaji wa majukumu yaKamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita tuliguswa na tukaanza mara moja jitihada zakuwapatia jengo hili ambalo litasaidia maofisa wa jeshi hili kufanya kazi kwaufanisi zaidi na kupunguza msongamano, hasa katika kipindi hiki cha ugonjwa waUVIKO-19 ambao unaweza kuepukwa kwa kupunguza misongamano kwenye maeneo yetu yakazi,” alisema Shayo.

 

Kamandawa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe (kulia) akitoa shukrani kwa Makamu waRais wa GGML anayeshughulikia miradi endelevu, Simon Shayo baada ya kupokeajengo jipya lililojengwa na kampuni hiyo kwa lengo la kuboresha huduma za kipolisimkoani humo.

Aidha, Kamandawa Polisi wa Mkoa wa Geita, Hendry Mwaibambe ameipongeza Kampuni ya GGML kwaufadhili huo kwani utasaidia zaidi kuongeza ufanisi wa shughuli za ulinzi nausalama Mkoani Geita.

 

“Kwaniaba ya Inspekta Generali wa Polisi nchini, nawapongeza kwa dhati kabisakampuni ya GGML kwa kuwa wadau wetu muhimu wa maendeleo, ikiwa ni pamoja nakutusaidia ujenzi wa ofisi hii ya kisasa yenye mahitaji yote muhimu.

 

“Tunatambuapia mchango wao mwingine wa kutupatia gari mapema mwaka huu. GGML wamekuwa piawakitufanyia matengenezo, kutupatia magurudumu mapya na mafuta kila maratunapohitaji msaada huo.

 

“Tunawahakikishiakuwa tutaendelea kusimamia ulinzi na usalama katika mkoa huu ili wananchi wote,ikiwa ni pamoja na GGML wemyewe waweze kuafnay shughuli zao kwa amani, usalamana tija kwa ajili ya uchumi na maendeleo ya nchi yetu,” alisema KamandaMwaibambe.

NAMWANDISHI WETU

Leave A Reply