The House of Favourite Newspapers

GGML Yathibitisha Yaendelea Kuisaidia Jamii ya Geita

0
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson (kulia) akikabidhi mkataba wa makubaliano Mpango wa uwajibika kwa jamii mwaka huu (CSR) kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (kushoto).

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) pamoja na Halmashauri ya Mji wa Geita mapema jana imesaini makubaliano ya utekelezaji wa Mpango wa kusaidia Jamii (CSR) kwa mwaka 2020 wenye thamani ya  Sh bilioni 9.2.

 

Makubaliano hayo yamethibitisha ahadi GGML kwa Serikali baada ya kutekeleza mabadiliko yaliyomo kwenye kifungu cha 105 cha Sheria ya Madini ambacho kinajumuisha utekelezaji wa Mpango wa uwajibikaji kwa jamii (CSR).

Baadhi ya maofisa kutoka kampuni ya GGML na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita wakisaini makubaliano hayo huku wakishuhudiwa na baadhi ya maofisa wengine.

Utekelezaji wa mpango huo wa CSR utanufaisha jamii ya Geita katika maeneo ya mazingira, miundombinu, afya, elimu na biashara ndogo na za kati (SMEs).

 

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel alielezea namna Serikali ya inavyothamini ushirikiano mzuri uliopo kati  GGML na jamii ya Geita.

 

Alisema GGML inajitahidi kusaidia Serikali za kuwa na maendeleo endelevu  ya jamii na uchumi katika jamii ya mji wa Geita.

Mkurugenzi wa Mji wa Geita, Mhandisi Modest Apolinary (kulia) na Mkurugenzi wa Wilaya ya Geita, Alli Kidwaka (kushoto) wakisaini makubaliano hayo.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson alisema hatua hiyo inatekeleza malengo ya kampuni hiyo kuendeleza ushirikiano na serikali za mitaa na jamii nzima kwa ujumla katika kutambua na kusimamia miradi muhimu kwa mustakabali endelevu wa mkoa wa Geita.

 

“Tunafurahi sana kuendeleza ahadi yetu kwa Serikali na jamii wenyeji. Katika mwaka huu wa tatu wa utekelezaji wa npanngo huu baada ya mabadiliko ya sheria ya madini, ni matumaini yetu kuwa tunaweza kuendeleza tulipoishia katika miradi iliyopita ili kuongeza tija na umiliki  kwa jamii lakini pia kuendelea kuahidi ushirikiano katika miradi endelevu ambayo itaendelea kuwepo  hata baada ya shughuli za mgodi.

Mkuu wa Sheria kutoka Kampuni ya AngloGold Ashanti – Geita Gold Mining Limited (GGML), David Nzaligo na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Richard Jordinson wakisaini makubaliano hayo.

“Tangu GGML ianzishwe, imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na serikali ya mkoa wa Geita kusaidia miradi kadhaa ya kijamii katika mkoa wa Geita kupitia ushirikiano baina ya Serikali na sekta binafsi (PPP) sanjari na mpango ya Kitaifa.

“Pamoja na tunu yake kuu ya kusaidia jamii ya Geita kuwa na maendeleo endelevu kijamii na kiuchumi ambayo yatabakia hata baada ya shughuli za uchimbaji kumalizika, pia kampuni imefadhili utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwamo usambazaji wa maji safi, uendelezaji wa shughuli za uchumi katika sekta za kiimo, ujenzi na huduma,” alisema.

NA MWANDISHI WETU

Leave A Reply