The House of Favourite Newspapers

Giannis hajalala kutolewa NBA

STAA wa Milwaukee Bucks, Giannis Antetokounmpo amesema amekuwa anakosa usingizi baada ya timu yake kutolewa kwenye Ligi ya NBA. Buck ilitolewa kwa jumla ya mechi 4-2 na Toronto Raptors kwenye fainali ya Kanda ya Mashariki ‘Eastern Conference’.

 

Giannis amedai amekuwa anakosa usingizi kwa muda mrefu sasa tangu walipofungwa kwenye mechi ya mwisho Jumamosi iliyopita.

 

Hata hivyo, Giannis amejifariji kuwa timu yao ilifanya vizuri licha ya kutolewa na Raptors “Ninachofariji ni kuwa watu wengi wamesifia kuwa tulicheza vizuri kwenye michuano hii.

 

Mashabiki wametukubali walikuwa wanasisimka kwa jinsi tulivyokuwa tunacheza,” alisema Giannis. Giannis anaamini kuwa timu hiyo itakuwa vizuri zaidi msimu ujao kuweza kufanya makubwa. Kivumbi cha fainali za NBA kinata zamiwa kuanza kesho kutwa Ijumaa wakati Toronto Raptors itakapoi karibisha Golden State Warriors.

Comments are closed.