The House of Favourite Newspapers

 Gigy Money aapa kubadilika, kukwepa marafiki

NAAPA kubadilika! Ndivyo alivyosikika mwanamuziki machachari kwenye gemu la Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ambapo amesema ahitaji tena marafiki micharuko kama alivyokuwa yeye zamani na hata akiona kuna dalili ya yeyote kumfuata, basi atamkwepa.

Gigy aliiyambia Za Motomoto ya Risasi kuwa, katika safari yake ya mabadiliko, ameamua kujiweka mbali na marafiki wasio na tija kwenye maisha yake, badala yake ametafuta wengine kabisa na kati ya hao wengi wametoka kanisani.

“Sasa hivi sitaki kabisa marafiki micharuko, yaani hawana nafasi kwangu na watazidi kunishangaa sana. Kwa kufanya hivyo, mambo yangu mengi yatabadilika,” alisema Gigy.

STORI:IMELDA MTEMA

Comments are closed.