The House of Favourite Newspapers

Utata wa mimba ya Kim Nana

UTATA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Video Queen Lilian Kessy ‘Kim Nana’ kuanika kitumbo chake kinachoonesha kina kiumbe ndani, kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo waliibuka watu na kudai kuwa ujauzito huo unawagusa wanaume wawili.

Wadau hao walishadadia kuwa, eti kuna uwezekano kitumbo hicho kinamhusu mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au mpenzi wake wa hivi karibuni, Tonny Albert ‘Tbway’, jambo lililoibua utata.

Awali kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kim Nana alitupia picha akiwa amevaa kigauni cheusi kilichombana na kuwafanya wanazengo waanze kutoa ya moyoni.

“Huyu Kim Nana siku hizi ana kitumbo kikubwa kweli, yaani huyu ana ujauzito na nasikia ujauzito huo una utata wa wanaume wawili; aliyekuwa mpenzi wake pamoja na Tbway,” alikomenti mmoja wa mashabiki anayejiita Husna Wakuache.

Baada ya ubuyu huo kuzagaa mtandaoni, Risasi Jumatano lilifanya jitihada za kumtafuta mwanadada huyo ili kupata ukweli ambapo alipopatikana alisema hawezi kueleza ni nani mhusika wa kibendi chake mpaka pale atakapokuwa tayari kuanika kila kitu.

“Mimi napenda watu wanavyohangaika kutaka kujua ukweli wa tumbo langu, ila mimi ndio najua nani ni mhusika na nani sio mhusika, waendelee kuwa na subira tu ipo siku nitamuweka wazi mhusika na watapata majibu ya maswali yao, kwa sasa wabaki na utata wao,” alisema Kim Nana.

Msanii huyo aliwahi kudaiwa kutoka na Diamond kabla ya baadaye kudaiwa kuhamia kwa Tbway, kwa sasa licha ya kuonekana ana mimba, lakini haijulikani nani baba kijacho.

STORI: MEMORISE RICHARD, RISASI MCHANGANYIKO

Comments are closed.