The House of Favourite Newspapers

Gigy na madai ya kutumia unga, bangi

0

GIGY (2)Stori: MAYASA MARIWATA

MUUZA nyago gumzo Bongo kutokana na matukio yake, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amedaiwa kuwa anatumia unga na kuvuta bangi ndiyo maana amekuwa akifanya vituko visivyoweza kufanywa na mwanamke anayejitambua.

Licha ya tabia yake ya kupiga picha za nusu utupu, kuropoka maneno yasiyo na staha, juzikati ilivuja video yake aliyojirekodi akivua nguo kabisaa, hali iliyowafanya wengi kuhisi ‘anapuliza moshi na kula sembe’.

Akifungukia madai hayo, Gigy alisema: “Hawajui tu akili zangu zikoje maana situmii hivyo vitu kabisa, huwa nafanya mambo mengi ya ajabu nikiwa mzima, kilevi ninachotumia ni pombe tu.”

Leave A Reply