The House of Favourite Newspapers

Giroud Kitakwimu Hatakiwi Kusemwa

OLIVIER Giroud ndiye mchezaji anayezungumziwa zaidi duniani kwa sasa, wengi hawamzungumzii kwa mazuri yake, bali mabaya. Ukikutana na watu watakuambia kuwa jamaa hajui soka, jamaa hajui kufunga mabao, jamaa hana uwezo na utasikia wengine wakisema kuwa jamaa anainyima timu yake makombe.

 

Ndiyo kauli za Watanzania wengi wajua soka, hawa wamekuwa wanafahamu soka kuliko watu wengine wengi duniani, ndiyo hao wanaweza kubishana kuanzia asubuhi hadi jioni na kusema kuwa Ronaldo hajui soka.

 

Giroud ametoka Ufaransa akiwa mmoja kati ya wachezaji mahiri, kumbuka wakati anajiunga na Arsenal alikuwa mfungaji bora kwenye Ligi Kuu ya Ufaransa akitokea kwenye kikosi cha Montpellier ya Ufaransa, kuna kocha ambaye anaweza kuacha kumsajili mfungaji bora? Nafikiri hapana, hata kama asin∆geenda Arsenal basi angeweza kwenda sehemu nyingine.

 

Makocha wanaofahamu kuhusu wachezaji, wengi wamekuwa wakiamini kuwa Giroud ni mchezaji mwenye uwezo wa juu sana. Mashabiki wa Arsenal hawataki kumsikia, wanaamini kuwa siyo mchezaji mahiri, lakini amekwenda Chelsea nao w a m e k u w a w a k i s e m a hivyo hivyo, hawataki kumuona.

Hawataki kumsikia, lakini kitakwimu Giroud anaweza kuwa hana mfano kwenye dunia ya sasa ya soka, huyo ni mchezaji aliyefanikiwa kwa kiwango cha juu sana kwenye soka.

 

Ni mchezaji ambaye huwezi kumfananisha na wachezaji wengi duniani, kuna jambo ambalo ameshawashinda hata Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, nalo ni kitendo cha kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia. Ronaldo na Messi hawajafanya hivyo, lakini Giroud ambaye anatajwa kuwa hana uwezo wa juu  ameshatwaa ubingwa huo,

lakini kumbuka kuwa Giroud amekuwa na mafanikio makubwa k u l i k o wachezaji wengi kwa kuwa tu anafahamu nini anachofanya.

 

M a f a n i kio makubwa ya mchezaji yeyote duniani ni kutwaa makombe, ndiyo, Giroud ana hazina ya makombe na amekuwa akiyatwaa mfululizo sana. Miaka mingi mfululizo kila mwaka Giroud amekuwa akitwaa mak o m b e , Giroud ametwaa mak o m b e kwenye k i l a m s i m u k u a n z i a msimu wa 2011/ 2012 hadi msimu huu wa 2017/2018. K i l a m s i m u a m e kuwa a k i t waa

kombe moja au mawili, bado kuna mtu anaweza kukaa na kusema kuwa Giroud siyo mchezaji mzuri. Kabla hajafika London akiwa na timu yake ya Montpellier, alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa msimu wa 2011/2012. Akiwa na Arsenal, amefanikiwa kutwaa makombe matatu ya FA na Ngao ya Jamii mara tatu, akaenda Chelsea akatwaa ubingwa wa FA msimu uliomalizika, lakini kumbuka kuwa mwaka huu pia ametwaa ubingwa wa Kombe la Dunia. Wengi wamebakiza kusema kuwa Giroud amemaliza Kombe la Dunia bila kupiga shuti hata moja langoni, lakini hawasemi a m e fanikiwa kitu g a n i , h a wasemi b a a d a ya msimu timu hiyo imevuna nini na yeye ameweka rekodi gani. Akiwa na Arsenal ambapo alikuwa akisemwa sana mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 253 na kufunga mabao 105, huku akiwa na heshima kubwa msimu wa 2015/2016 alipofunga mabao 24. Maisha ya Giroud ambaye ni mshambuliaji wa mwisho kwenye timu zote anazochezea yamekuwa yakionyesha kuwa ameshafunga mabao 201 kwenye michezo 482, wastani ambao unaonekana kuwa mzuri kwa mshambuliaji huyo. Amebakiza mambo mawili, moja kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na jambo la pili ni kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini kitakwimu jamaa yupo vizuri kuliko maneno ya wengi.

Comments are closed.