The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI FEBR 25: Mbele ya RC MWANRI, Makamu wa RAIS Awapa Maagizo TABORA! – VIDEO

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoa wa Tabora kutunza mazingira ili kufanikisha ujenzi wa mradi wa stiglers Gorge uliopo mkoani Morogoro katika kufanikisha kauli mbiu ya kuijenga Tanzania ya uchumi wa viwanda.

Mama Samiah ameyasema hayo katika Kongamano la kujadili mustakabali wa mazingira mkoani Tabora ambapo matumizi ya kuni na mkaa yameonekana kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira mkoani humo.

Aidha Makamu wa Rais ameainisha baadhi ya shughuli za kibinadamu zinazoathiri mazingira, huku akisema kuwa ni jukumu la kila mtanzania kulinda mazingira ili kufanikisha lengo la serikali la kuelekea uchumi wa kati.

Naye mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza katika kongamano hilo amesema kuwa Lengo la kongamano hilo ni kuweka hali nzuri ya mazingira ndani ya mkoa huo. Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria kongamano hilo wameelezea hali ya mazingira ya mkoa huo ilivyo nakufafanua namna watakavyoweza kutunza mazingira.

Katika kongamano hilo makamu wa rais amezindua mnara wa kumbukumbu shughuli za uhifadhi mapori ya akiba na misitu pamoja na kampeni ya upandaji miti ya kuifanya Tabora kuwa mkoa wa kijani.

Comments are closed.