The House of Favourite Newspapers

GLOBAL YATOA SHUKURANI KWA WASOMAJI MAGAZETI DAR LIVE

Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo akizungumza na mavenda (hawapo pichani).
Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akijibu maswali yaliouliza na mavenda (hawapo pichani) pembeni yake Eric Shigongo akimsikiliza.
Mmoja kati ya mavenda akiuliza swali kwa niaba ya wenzake.
mavenda na baadhi ya wafanyakazi wa Global wakifuatilia kikao kwa makini.
Mavenda waliodumu kwa zaidi ya miaka 20 katika kuuza magazeti ya Global wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuitwa mbele na Eric Shigongo.
Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (katikati) akifuatilia kwa makini kikao cha mavenda kulia kwake ni Mhariri wa Risasi Jumamosi, Hamida Hassan na kushoto kwake ni Mhariri Msaidizi wa Spoti Xta, Samson Mfalila
Eric Shigongo akimsikiliza mtangazaji wa Global TV Online, Junior Msongo.
Mavenda wakipata chakula mara baada ya kumalizika kwa kikao.
Saleh Ally akipakuliwa chakula.
Eric Shigongo akipakuliwa chakula
Mmoja wa mavenda akitoa uhushuda wake wa kuuza magazeti ya Global tangu 1999 na kufanikiwa kujenga nyumba mbili.

Wasomaji pamoja na mavenda wa magazeti wamejitokeza kwa wingi katika Tamasha la kuwashukuru wasomaji linalotambulika kama Tusua Maisha na Global lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa Magazeti ya Amani, Championi, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda pamoja na Uwazi.

 

Katika tamasha hilo lililohudhuriwa na mamia ya wasomaji, lilianza kwa mavenda kuwa na kikao na viongozi wa Global Publishers ambapo walitoa changamoto zao na pongezi kwa kuwakutanisha pamoja.

 

Mkurugenzi wa Global Publishers, aliwashukuru wote waliojitokeza na kuwaita baadhi ya mavenda waliokuwa pamoja na Magazeti ya Global tangu yanaanzishwa mwaka 1998.

 

“Nawashukuru wote kwa kuacha kazi zenu na familia, mmekuwa muhimu sana kwani bila mavenda Global isingekuwepo. Tumekuja hapa kuwasikia, mseme kila kitu tutafanyia kazi.

 

“Kuna wengine wameleta maoni yao ya tisheti na kofia, zawadi kila wiki kwa venda watakaofanya vizuri hilo tutalifanyia kazi haraka iwezekavyo kuanzia wiki ijayo. Tumeshirikiana nanyi kwa muda mrefu, tulishawahi kutoa shilingi milioni 7 katika saccos yenu kiufupi uhusiano wetu umekuwa karibu sana,” alisema Shigongo.

 

Naye Meneja wa Global, Abdallah Mrisho alzungumza kilichofanya hadi magazeti ya Global kupandishwa bei ambapo alisema, suala lililochukuliwa halikwepeki kwani kila kampuni ya gazeti itapandisha bei ni suala la muda tu.

 

“Tunazingatia ubora wa kazi, tumekuja na promosheni ya kujishindia pikipiki na zawadi nyingi na hii ni kwa ajili ya kuendelea kuwa na wasomaji wetu, ” alisema Mrisho.

 

Wapo mavenda waliotoa ushuhuda wao kuwa magazeti ya global yamekuwa yakiendesha maisha yao ambapo mmoja wa mavenda alitoa ushahidi wa kujenga nyumba mbili moja maramba mawili na moja Kibaha.

 

Baada ya kikao hicho, viongozi wa Global wakiongozwa na Shigongo walielekea kupata chakula cha pamoja pamoja na kupata burudani ya muziki kutoka kwa Man Fongo, Juma Nature pamoja na Roma Mkatoliki.

PICHA: RICHARD BUKOS

Comments are closed.