The House of Favourite Newspapers

GLOBAL YATUNUKIWA TUZO NA DSJ

 

Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas (kulia) akimkabidhi Tuzo ya Heshima, Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalallah Mrisho kufuatia mchango mkubwa wa Global katika kuwaendeleza wahitimu wa chuo hicho ikiwemo kuwapa ajira na nafasi za kujifunza kwa vitendo ‘Field’.

Chuo cha Uandishi wa habari cha Dar es Salaam (DSJ) jana Ijumaa Dec 21 kilifanya Mahafali yake ya 23 na kutuo tuzo mbalimbali kwa wadau wake, wakiwemo Global Publishers kwa kutambua mchango wake katika kuwapa nafasi wanafunzi wake kufanya mafunzo yao kwa vitendo.

Katika hotuba yake, Mkuu wa Chuo hicho Joachim Rupepo, mbele ya wahitimu 156 na na mgeni rasmi, aliishukuru Kampuni ya  Global Publishers kwa kuwapa nafasi ya kujifunza kwa vitendo pamoja na kuwapa ajira wanafunzi wengi wanaotoka chuoni bila vikwazo, ukilinganisha na baadhi ya makampuni mengine ambayo hutoa nafasi hizo kwa malipo.

Wahitimu wakijimwaya kwa muziki kwenye hafla hiyo.

Wahitimu wa kozi ya utangazaji wakionesha umahiri wao wa kutangaza.

Wahitimu na wageni waalikwa wakifuatilia matukio.
Wahitimu wakisoma risala.

(PICHA / HABARI:  RICHARD BUKOS)

Comments are closed.