The House of Favourite Newspapers

GlobalUpdates: Madereva Daladala Kituo cha Simu 2000 Wagoma

0
Hali ilivyo katika kituo Cha Daladala cha Simu 2000.

 

#GlobalHabariUpdates: Madereva wa daladala kituo cha Simu 2000 (Mawasiliano) kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam wamegoma kutoa huduma kuanzia leo Jumatatu, Agosti 21 alfajiri wakipinga ongezeko la ushuru kituoni hapo kutoka Sh 500 hadi Sh 1,000.

 

Madereva na makondakta wakiwa wamekusanyika.

Wakizungumza na Global TV Online, madereva hao wamelalamikia kitendo cha Manispaa ya Ubungo kuwapandishia gharama za ushuru wakati hali ya uchumi na biashara kwa ujumla ni ngumu kwao.

 

Abiria wakikosa usafiri.

“Takribani mwezi mmoja uliopita katibu wa soko alituletea notisi ya mwezi mmoja ikieleza kuwa ushuru utapanda kutoka Sh 500 hadi Sh 1,000, sisi tulikataa na tukawasilisha malalamiko yetu kwa Mkuu wa Mkoa, lakini kabla ya maamuzi jana tumeletewa tena vipeperushi vikieleza kuanzia leo gharama ya ushuru ya Sh 1,000 itaanza kutolewa, jambo ambalo hatujaafikiana nalo,” alisema Husein mmoja wa madereva hao.

 

Madereva wakiwa wamekusanyika wakati wamepaki magari yao.

“Tulichokiamua sisi madereva hakuna kuingiza gari stendi wala kubeba abiria hapa Mawasiliano hadi kilio chetu kiifikie serikali na maamuzi sahihi yatolewe. Hatuwezi kunyanyasika kwenye nchi yetu. Tunapandishiwa ushuru kwa asilimia 100 ghafla.

 

Hali halisi kituoni hapo.

“Pesa yenyewe tunayopata ni ndogo, pia gaharama za ushuru wa stendi mabosi wetu hawazitambui, wanachotaka hesabu zao zitimie. Kwa kweli hatukubali. serikali watuangalie na sisi ni Watanzania kama wengine, ” alisema dereva Tumaini.

 

Hali halisi kituoni hapo.
Mmoja wa wasafiri aliyefika kituoni hapo akielezea adha alivyopata baada ya kukosa usafiri.

Kwa upande wao abiria wamelalamikia kitendo cha kukosa ufasiri kituoni hapo tangu alfajiri jambo ambalo limewafanya kuchelewa kufika kwenye maeneo yao ya kazi ilihali kituo hicho wanakitegema kwa usafiri muda wowote.

 

 

NA DENIS MTIMA | GPL

 

===================

VARANGATI: Mgomo wa Daladala DAR Yasimama, Madereva Watoa Yamoyoni

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Sikiliza Hadithi za Mtunzi Eric Shigongo Hapa

Leave A Reply