The House of Favourite Newspapers

Guardiola Ahofia Liverpool Kuvunja Rekodi za City

0

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, ameanza kupata wasiwasi kuwa mwendo huu wa Liverpool unaweza kuvunja rekodi nyingi walizoziweka.

City ya Guardiola ilikuwa timu ya kwanza kufikisha pointi 100 kwenye Premier ilipotwaa ubingwa miaka miwili iliyopita.

 

Wakati wa ubingwa wa msimu wa 2017-18, pia waliweka rekodi ya ushindi mwingi (32), mabao mengi (106) na ushindi mwingi mfululizo kwenye msimu mmoja wa Premier (18).

 

Pia waliifikia rekodi ya kutwaa ubingwa mapema zaidi walipoubeba wakiwa wamebakiza mechi tano. Na waliutwaa wakiwa wametengeneza gepu kubwa dhidi ya timu ya pili, Manchester United.

 

Lakini msimu huu, kikosi cha Jurgen Klopp kinaelekea kuvunja rekodi nyingi kati ya hizo, ikiwa kimeshashinda mechi 22 kati ya 23.

 

Guardiola amesema: “Rekodi zipo ili zivunjwe. Tulivunja wakati watu wengine wakifikiri haiwezekani kuvunja. Hivi karibuni au baadaye itatokea, historia inatuambia hivyo.” Liverpool kwa sasa inaonekana kama haifungiki, na Guardiola ameongeza: “Siyo rahisi kuwafunga kwa sasa, wamepata njia ya kushinda mechi zao.”

MANCHESTER, England

Leave A Reply