The House of Favourite Newspapers

Mafuriko China yawakwepesha Guardiola na Mouinho

0

man+unitedBEIJING, CHINA

MECHI ya kirafiki ya kujiandaa na msimu kati ya mahasimu wa jiji la Manchester, Man United na Man City iliyokuwa ipigwe usiku wa kuamkia leo imeahirishwa.

Mechi hiyo iliyokuwa ipigwe nchini China imeahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kuufanya uwanja ujae maji, mvua hizo zimesababisha vifo vya watu zaidi 200 mpaka sasa huku wengine mamia wakiwa majeruhi na wengine mamia hawajulikani walipo huku nyumba zaidi ya 68,000 zikiwa zimeharibiwa vibaya na watu milioni 16 wakikoswa makazi.

Bad weather led to the cancellation of the Manchester derby at the Bird's Nest in Beijing, much to the frustration of fans

Uwanja wa Beijing uliokuwa utumike kwa mechi hiyo uliwafanya makocha, Jose Mourinho na Man United na Pep Guardiola wa Man City wote kutoafiki kuchezwa mwechi hiyo.

Mourinho kwa upande wake aliuelezea uwanja huo kuwa uko katika hali mbaya wakati Guardiola alisema kitu ambacho asingekipenda ni kuona wachezaji wakiumia kutokana na uwanja huo.

rainfall china Baadaye viongozi wa City na United walisema kuwa waandaaji wa mechi hiyo waliamua kuiahirisha huku habari za watabiri wa hali ya hewa zikidai kwamba mvua hizo zingeendelea leo Jumatatu hali ambayo ilizifanya timu hizo kubadili viwanja vya mazoezi.

rainfall kills 87 chinaMashabiki zaidi ya 500,000 walitaajiwa kuingia uwanjani hapo kushuhudia mpambano huo.

Mechi hiyo ilitajwa kuwa ni mwanzo wa vita ya soka ya makocha, Mourinho na Guardiola ambao wamekuwa na uhasama wa muda mrefu.

Leave A Reply