The House of Favourite Newspapers

Gwiji wa Everton Amwaga Vifaa kwa Watoto, Aitabiria Ubingwa Gor Mahia

Yakubu Aiyegben (wa tatu kushoto) baada ya kukabidhi vifaa hivyo.

GWIJI wa Soka Nigeria na Everton FC ya Uingereza, Yakubu Aiyegben amekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa watoto wa vituo mbalimbali vya kukuzia vipaji nchini Kenya.

Akizungumza na Mhariri wa Gazeti la Michezo la Championi, Saleh Ally ambaye pia ni Mchambuzi wa michezo wa Global TV Online.

Program hiyo kufanywa mara kwa mara na Everton ikilenga kusaidia kinua na kukuza vipaji vya watoto hao ambao watakuwa wanasoka wa baadaye.

Mbali na hayo, Yakubu ameitabiria timu ya Gor Mahia ya Kenya kubeba Ubingwa wa Kombe la SportsPesa Super Cup 2018 dhidi ya Simba Sc ya jijini Dar es Salaam.

Akipiga stori na Global TV Online, Yacob amesema Gor Mahia ina nafasi kubwa kwa kuwa inacheza kwa ushirikiano mkubwa kwenye kukaba na kushambulia.

Fainali ya SportsPesa Super Cup 2018 inatarajiwa kupigwa kesho Jumapili huko Nakuru nchini Kenya ambapo Bingwa ataibuka na mkwanja lakini pia atapata fursa ya kwenda nchini Uingereza kucheza mechi na timu ya EPL inayodhaminiwa na SportPesa ya Everton anayoichezea Wayne Rooney.

 

Picha na Musa Mateja | Global TV Online, Kenya.

Comments are closed.