The House of Favourite Newspapers

Hali ilivyo Mwanza kuelekea maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru

0

Kesho Desemba 9, 2019 Tanzania Bara itasherehekea miaka 58 tangu kupata uhuru wake na miaka 57 ya Jamhuri, tayari viongozi mashuhuri wameshawasili jijini Mwanza kwa sherehe hizo.

 

Hali ya hewa jijini hapa ni tulivu huku  mvua ya hapa na pale imekuwa ikinyesha kutwa mara tatu mpaka nne, hivyo kuna ubaridi katika jiji hili ambalo linakwenda kuiwakilisha nchi katika kusherehea Ssherehe hizi za Uhuru.

 

Wakati sherehe hizo zikitarajia kufanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa mitaa mbalimbali ya jiji hili imepambwa kwa bendera za taifa za nchi yetu hali inayolipendezesha jiji la Mwanza.

Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo anatarajia kuzindua miradi minne inayotekelezwa na serikali eneo la Bandari ya Mwanza Kusini.

Miradi itakayowekewa mawe ni pamoja na Ujenzi wa Meli mpya ambao utagharimu  kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 89, mradi wa pili  ni ujenzi wa chelezo kitakachogharimu Bilioni 36, mradi wa tatu ni ukarabati mkubwa wa meli ya MV Victoria ambao utagharimu bilioni 22.7 mpaka kukamilika kwake na mradi wa nne ni ukarabati wa meli ya MV Butiama ambapo thamani ya ukarabati wake ni bilioni za kitanzania 4.9 ambapo wakandarasi wa miradi hii ni pamoja na

 

Na Johnson James -GPL- MWANZA.

Leave A Reply