The House of Favourite Newspapers

Hall: Ubingwa ligi kuu siyo kazi rahisi

0

_70995516_hall_Kocha wa Azam, Stewart Hall.

AZAM FC imepata ushindi wa kwanza tangu irejee kutoka michuano ya Kombe la Mapinduzi, lakini kocha wake Stewart Hall amesema ni ngumu kuijua mapema timu itakayochukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara kutokana na ushindani mkubwa uliopo.

Jumatano iliyopita, Azam iliifunga Mgambo JKT mabao 2-1 na kufikisha pointi 39 sawa na Yanga lakini ipo nafasi ya pili ikizidiwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Hall alisema: “Sioni dalili za kupatikana bingwa wa mapema kutokana na ushindani mkubwa katika mechi tunazocheza kwa kuwa kila timu tunayokutana nayo inacheza kwa kukamia.
“Ligi bado ngumu kadiri siku zinavyokwenda ndiyo timu zinazidi kuimarika kwa sababu hazitaki kuwa wasindikizaji kwa kufungwa na kila timu.
“Bado ni kazi kubwa kutabiri nani atakuwa bingwa kutokana na kwamba wapinzani wetu Yanga nao wanapambana kama sisi.
“Naamini bingwa ataanza kuonekana katika mechi chache kabla ya kumalizika kwa ligi lakini siyo sasa,” alisema Hall, raia wa Uingereza.

Leave A Reply