The House of Favourite Newspapers

Halotel Yasherehekea Siku ya Wanawake Duniani Kwa Kutembelea Kituo Cha Watoto Yatima Malaika

0
Picha ya pamoja wa katikati ni mkuu wa kituo hicho Bi. Najma Manji akikabidhiwa vitu hivyo na wafanyakazi wa Halotel siku ya leo Machi 7,2024.

Halotel kuonesha dhamira yao katika kujali jamii iliweza kutembelea kituo cha watoto yatima cha Malaika kilichopo Mwananyama – Mango Garden katika kukaribisha sherehe za sikuukuu ya Wanawake mwaka 2024.

Halotel Tanzania imetoa msaada kituo cha watoto Yatima Malaika kilichopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam Katika kuheshimu na kukaribisha sikukuu ya wanawake na kutambua umuhimu wa mwanamke katika jamii yetu, Halotel imeamua kuwashika mkono wanawake ambao wameazisha kituo hiki cha watoto Yatima.


Katika tukio hilo, Halotel Tanzania imeweza kujumuika na watoto hao katika michezo mbalimbali ya kujifunza. ‘Tunaamini katika nguvu ya kujali na kurudisha katika jamii hususani kwenye siku kubwa kabisa ya sikukuu za wanawake’ alisema Madam Sharon
Kessy ambaye ni Ofisa kutoka kitengo cha Huduma kwa wateja.

‘Kwa kuwatembelea watoto hawa tunatambua umuhimu wa kuwaelimisha na kuwatia moyo kujikita katika elimu ili kuweza
kujikwamua katika maisha.’ aliongeza Madam Sharon.

Halotel Tanzania kwa kutembelea Kituo hicho inaendelea kuonesha dhamira yao katika kujali jamii imetoa zawadi ya mifuko 600 ya mchele, vifaa vya usafi pamoja na Taulo za kike ambavyo kwa pamoja ameweza kukabidhiwa msimamizi wa kituo hicho cha watoto yatima cha Malaika.


“Halotel Tanzania inapenda kuwashukuru na kuwatia moyo wanawake wanaosaidia watoto hawa katika hiki kituo cha watoto Yatima cha Malaika, lakini pia kuwatia moyo wanawake wote wanaojitahidi kujishughulisha kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali katika jamii Yetu”.

Picha ya pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Halotel baada ya kukabidhiwa msaada ikiwa ni katika kuelekea kilele cha simu ya Mwanamke duniani.
Leave A Reply