The House of Favourite Newspapers

Hamadombe, Mzee Yusuph hapatoshi Dar Live

0

Mzee Yusuf akiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa My Valentine  ndani ya Dar Live.

Na Imelda Mtema,

Dar es Salaam

LEO Jumamosi kwenye Ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem jijini Dar, kutakuwa na burudani ya aina yake itakayotolewa kwa pamoja na Bendi ya Hamadombe na Mzee Yusuph, Mfalme wa Taarab.

Kwa mujibu wa mmiliki wa Hamadombe, Fatuma Makame, bendi yake sasa ina miaka minne na ipo fiti kutoa burudani sambamba na Mzee Yusuph katika onyesho hilo.

“Kwa kweli vijana wangu wapo vizuri na kila siku wanapambana kufika mbali zaidi, naamini watafanya kitu kizuri ambacho kitakubaliwa na mashabiki wa muziki,” alisema Fatuma, maarufu kama Joanita.

Hadi sasa Hamadombe wametoa vibao kadhaa vikiwemo She is Beautiful, Siyataki Mapenzi na Bila Haya ambacho kipo mbioni kutolewa video yake.

Leave A Reply