The House of Favourite Newspapers

Hamisi Bss: Nimesafisha Macho

0

MSHIRIKI wa Shindano la Bongo Star Search (BSS), Hamisi Saidi amesema hata kama hatonyakuwa kitita cha shilingi milioni 20 lakini atakuwa amesafisha macho kwa kiasi kikubwa sana na hawezi kujutia nafasi hiyo aliyoipata hata.

 

Akipiga stori na Wikienda, Hamisi alieleza kuwa hakuna anayejua nafasi aliyoipata imeusafishaje moyo wake kwa kiasi kikubwa na kamwe hawezi kusahau kipindi hiki katika maisha yake yote aliyoishi hapa duniani.

 

“Nimeona vitu vingi ambavyo sijawahi kuona katika macho yangu tangu nazaliwa, hakika nimesafisha macho yangu. Hata kama sitashinda, kuna vitu vingi sana nitakuwa nimejifunza nikiwa ndani ya BSS, na hata kuonana uso kwa uso na Madam Ritha kwangu ilikuwa ni ndoto kubwa,” alisema Hamisi.

Leave A Reply