Hamisi wa BSS: Harmonize Nisamehe, Nilidhani Nimetoboa

STORI zinazozungumza sana kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu aliyekuwa mshiriki wa Mashindano ya Kusaka Vipaji maarufu kama Bongo Star Seach (BBS), Hamisi wa BSS aliyejipatia umaarufu mwaka juzi 2019, kupitia mashindano hayo amemwaga machozi kwa bosi wa Lebo ya Konde Gang, Harmonize huku akiomba msaada kutoka kwa msanii huyo.
Hamisi ameenda mbali zaidi kwa kusema kama amemkosea Harmonize basi anaomba amsamehe kwani mwanzo alionesha nia ya kutaka kumsapoti wakati alipokuwa kwenye mashindano.
“Ningeomba sana anisaidie, ujue mpaka mtu anafikia hatua ya kulia kwa ajili ya kuomba msaada sio poa, anisadie kwa chochote kile hata kwa wimbo mmoja au video tu kwa sababu anajuana na watu wengi, alivyosemaga kwamba atanisaini na kunisaidia nilidhani nimeshatoboa au kama nimemkosea naomba anisamehe,” ameeleza Hamisi.

