The House of Favourite Newspapers

Hamorapa: Hata Waniue Mtoto wa Amber Lulu Ni Wangu

0

PAMOJA na kudaiwa kutekwa kisha kutiwa mbaroni kufuatia kudai mtoto wa msanii wa Bongo Fleva, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’ aitwaye Ariana aliyejifungua hivi karibuni kuwa ni wa kwake, msanii chipukizi, Omary Said ‘Hamorapa’ anasisitiza; “Hata waniue mtoto ni wangu!’Hamorapa alikamatwa na Polisi juzi, Jumamosi katika Hoteli ya Kebbys iliyopo Mwenge jijini Dar, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya sakata hilo.

 

Kukamatwa kwa Harmorapa kulitokana na kauli yake aliyoitoa akidai kuwa mtoto wa Amber Lulu ni wa kwake kwani wanafanana.

 

Baada ya kauli hiyo, mzazi mwenza wa Amber Lulu aliyetajwa kwa jina moja la Botion alimbana Hamorapa ambaye alikana na kusema kuwa mtoto huyo si wake.

Hata hivyo, pamoja na kubananishwa na jamaa huyo, baadaye Hamorapa alijirekodi tena kipande cha video akisema amenyanyaswa na kudhalilishwa na Botion na wenzake hivyo akasisitiza kuwa mtoto huyo ni wa kwake na atazungumza na wanahabari kuanika ukweli halisi, lakini wakati akiendelea kuzungumza na wanahabari ndipo Botion alitua na Polisi kisha wakamkamata na kumpeleka Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) jijini Dar.

 

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilizungumza na Hamorapa akiwa kwenye gari la Polisi mara tu baada ya kutiwa mbaroni ambapo aliendelea kusisitiza;“Hata kama nitauawa mtoto ni wangu, mimi siyo mjinga hata kidogo.

 

“Ukweli ni kwamba mtoto ni wangu na yeye (Amber Lulu) anajua hilo, mimi siyo mwendawazimu.

Baadhi ya watu wanashauri kuwa, ni vyema kukafanyika kipimo cha vinasaba (DNA) ili ukweli upatikane.Kwa mujibu wa Hamorapa, yeye na Amber Lulu waliwahi kuwa wapenzi siku za nyuma na ushahidi anao.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply