The House of Favourite Newspapers

Hans Poppe awabwaga Vital’O kwa KO

0

POPE1.jpg

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe.

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema Vital’O ya Burundi ni watu waliokosa ustaarabu na ni kama wamevamia jambo kuhusiana na mshambuliaji Laudit Mavugo.

laudit-mavugo-simba-2016_112df1z9vgamx1p9udfi200uzd

Mshambuliaji Laudit Mavugo akiwa ndani ya jezi ya Simba.

Vital’O ilijumuisha jina la Mavugo katika usajili wake mpya msimu ujao na kulipeleka kwenye Shirikisho la Soka la Burundi (FFB) ikisema bado ina mkataba naye.

Hans Poppe ameliambia Championi Ijumaa kwamba, Mavugo si mali ya Vital’O kama watu wanavyoamini, badala yake ni mchezaji anayemilikiwa na Klabu ya Solidarity ya nchini Burundi.

“Nashangazwa sana na Vital’O kukosa ustaarabu katika hili, Mavugo si mchezaji wao. Tayari tumemsainisha lakini tunaendelea na klabu yake ya Solidarity ambayo ndiyo ilimlea na kwa sheria za Burundi, ndiyo inammiliki.

“Alikwenda kucheza Vital’O kwa mkataba kama wa miaka miwili hivi. Sasa amemaliza, sisi tumefika hadi katika shirikisho la Burundi na wametupa maelezo ambayo ni sahihi.

“Inawezekana Vital’O walitaka kuongeza naye mkataba na imeshindikana. Sasa itakuwa ni vizuri sana wakafuata utaratibu, huyu si mchezaji wao,” alisema Hans Poppe.

Hata hivyo, Championi Ijumaa lilimtafuta, Rais wa Vital’O, Benjamin Bikolimana kulizungumzia suala hilo ambapo alisema: “Ni kweli tulikuwa na mpango wa kutuma jina la Mavugo kwa ajili ya kumtumia katika msimu ujao lakini leo (jana) asubuhi tumezungumza na Simba kuhusiana na hilo suala.

“Simba ni ndugu zetu na tumefikia pazuri, hatulitumi tena na sasa tupo kwenye mchakato wa kukamilisha ITC yake (Mavugo) kwa ajili ya kuichezea Simba msimu ujao na muda wowote kuanzia sasa tutakamilisha huo mpango.”

Leave A Reply