The House of Favourite Newspapers

Hao Simba Walivyoipania Gwambina Leo Mkapa Stadium

0

BIG bosi wa benchi la Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck ameweka wazi kwamba anaingia kwa umakini kwenye mechi yao na Gwambina FC licha ya kwamba wamekuwa na maandalizi mazuri.

 

Kocha huyo ameongeza umakini ambao anaingia nao ni kwa sababu ya kutotaka kupoteza pointi mbele ya wapinzani wake hao.

 

Mbelgiji huyo ataiongoza Simba kwenye mechi ya nne ya Ligi Kuu Bara kwa msimu huu dhidi ya Gwambina FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Kocha huyo amesema kuwa licha ya kwamba walicheza mechi moja ya kujiandaa na mechi hiyo lakini hilo haliwafanyi kutoingia kwa tahadhari mbele ya wapinzani wao hao.

“Tulicheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya African Lyon lakini haijatosha bado kutuaminisha kwamba tuko vizuri licha ya kuwa kila mchezaji kuonyesha uwezo wake mkubwa kwenye nafasi aliyocheza.

 

“Tunataka kufanya vizuri kwa mara nyingine kwenye mechi hii kwa sababu ya kufikia lengo letu la kutwaa kila pointi kwenye mechi zetu zote za hapa karibuni,” alisema Mbelgiji huyo.Naye Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema kikosi hicho kimejiandaa vyema kuhakikisha ushindi unapatikana licha ya ugumu wa mchezo huo.

“Kikosi chetu kipo kamili kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Gwambina, mpaka sasa tumefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huu kwa kuwa tunajua mchezo utakuwa mgumu kutokana na matokeo ambayo wapinzani wetu wameyapata kwenye michezo iliyopita.

 

“Tunataka kufanya vizuri kwa kuwa tanacheza kwenye uwanja wetu wa nyumbani tena mbele ya mashabiki wetu hivyo mpango wetu mkuu ni kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu.

 

”Kwa upande wake kocha mkuu wa klabu ya Gwambina, Fulgence Novatus alisema: “Tumepoteza mchezo wetu uliopita dhidi ya Ruvu Shooting na kufanya tusalie na pointi moja pekee jambo ambalo sio zuri kwetu. “Tunajua Simba ni timu bora lakini tutapambana ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo huu.

Stori: Said Ally na Joel Thomas

HARMONIZE na SKIBI/ COUNTRY BOY /Akishusha MICHANO ya HIPHOP LIVE JUKWAANI, UTAPENDA

Leave A Reply