The House of Favourite Newspapers

Hapa Ndipo Alipolala Akwilina Akwilini- Video

MWILI wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini umepumzishwa jana Ijumaa nyumbani kwa wazazi wake katika Kijiji cha Olele wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro huku simanzi na vilio vikitawala wakati wa safari ya mwisho ya msomi huyo.

Mwanafunzi huyo alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema).

Comments are closed.