The House of Favourite Newspapers

Happy Birthday Nyemo Chilongani

0

_PL_5235Mwandishi wa habari na hadithi kutoka Global Publishers, Nyemo Chilongani.

Na Mwandishi Wetu
Hatimaye mwandishi wa habari na hadithi kutoka Global Publishers, Nyemo Chilongani anajiandaa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo nyumbani kwao Tandale. Nyemo ambaye anatamba na simulizi mbalimbali kwenye magazeti kama Ijumaa, Wikienda, Championi na Uwazi amefanikiwa kutimiza miaka 27 leo hii.
Akizungumza na mwandishi wetu, Nyemo ambaye kwa sasa anakimbiza na hadithi nyingi amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumlinda siku zote tangu kuzaliwa kwake mwaka 1990 mpaka leo hii.
“Ni jambo la kumshukuru Mungu. Muda umekwenda sana, unapotimiza miaka fulani, hiyo ni alamu ya kukwambia kwamba unatakiwa kufanya jambo fulani la kimaendeleo ambalo hukulifanya kabla. Nawashukuru wazazi wangu pia, marafiki na wale wote ambao wameniwish siku ya leo, wamenifanya nijisikie kuthaminiwa,” alisema Nyemo ambaye anatarajia kutoa Kitabu cha Jini Mauti hivi karibuni.

Leave A Reply