The House of Favourite Newspapers

Harmonize na Kajala Wanakula Bata za Hatari, Hawana Habari na Tozo   

0

 

Harmonize na Kajala

KAJALA na Harmonize hawana habari na tozo, wanakula bata hatari maisha wanayoishi mastaa Kajala Masanja na Rajabu Abdul ‘Harmonize’ ni kama vile sio Wabongo, wanaishi kama mbele vile.

 

Suala la kwenda mapumzikoni katika mbuga za wanyama kwa ajili ya kupumzisha akili sio mpaka waandikiwe na daktari, wanafanya hivyo mara kwa mara.

 

Safari hii wawili hao wamenekana wakiwa hifadhi ya Taifa Manyara national park wakiwa wanakula maisha ambapo  walikuwa wawili kwenye swimming pool pamoja na mpiga picha wao ambaye hajaonekana pichani.

Harmonize na Kajala wanakula bata

Kajala kuna wakati alikuwa na kigauni cha uchokozi kabla hajabaki na kinguo maalum cha kuogelea ambacho kinaacha sehemu kubwa ya mwili wake wazi.

 

Baadhi ya maoni kwenye picha hizo ambazo Kajala kaziposti kwenye ukurasa wake wa Instagram, wapo waliompongeza lakini wengine wakiuliza kama wao hawajaguswa na makali ya tozo.

 

Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao.

 

 

Leave A Reply