The House of Favourite Newspapers

Harry Kane Ndiyo Basi Tena

STRAIKA wa Tottenham, Harry Kane yupo kwenye nafasi mbaya ya kurejea uwanjani msimu huu kutokana na tatizo la kifundo cha mguu linalomsumbua. Kane amepata majeraha hayo wakati Premier League ikielekea mwishoni na klabu yake inamhitaji huku akiwa anasubiriwa kuiongoza England katika michuano ya UEFA Nations League, Juni, mwaka huu.

 

Alifanyiwa kipimo cha mguu wa kushoto Jumatano iliyopita na ikaonekana amepata tatizo kwenye mfupa, hivyo anaweza kukosa michezo yote iliyosalia ya msimu huu wa 2018/19. Ikumbukwe kuwa, Kane aliumia wakati akiwania mpira na Fabian Delph wa Manchester City, Jumanne iliyopita katika
michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Klabu ya Tottenham ilitoa tamko kwa kusema: “Tunathibitisha kuwa baada ya uchunguzi Harry Kane ana tatizo la mfupa katika mguu wa kushoto. “Anaendelea kufanyiwa uchunguzi na wataalam, tatizo la sasa linafanana na lile lililomtokea Januari, mwaka huu.” Alipopatwa na tatizo la Januari alitakiwa kuwa nje kwa muda wa miezi miwili lakini alikuwa nje kwa muda wa wiki tano. Wakati huohuo, staa wa timu hiyo, Dele Alli aliyepata jereha la mkono katika mchezo dhidi ya Man City imethibitishwa kuwa amevunjika sehemu ya mfupa wa mkononi.

Comments are closed.