The House of Favourite Newspapers

HATIMAYE! LINAH MAHABA LIVE NA BWANA MPYA

BAADA ya kuachana na baba mtoto wake aliyejulikana kwa jina moja la Mchomvu, staa wa kike wa Bongo Fleva, Estalina SangaLinah’ amejiachia ‘live’ na jamaa anayesemekana kuwa ni bwana’ke mpya ambaye jina halikupatikana mara moja.

 

Tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita mjini Iringa ambako kulikuwa na ile shoo kubwa ya Wasafi Festival iliyofanyika kwenye Uwanja wa Samora.

 

Linah aliyeachana na baba mtoto wake miezi kadhaa iliyopita alionekana kwa mara ya kwanza na mwanaume mwingine ambapo gazeti hili liliwashuhudia wakiwa wamegandana kama ruba kwenye kila kona mjini Iringa.

 

Mbali na kugandana muda wote, hata mikao yao ya kimahaba ilikuwa inaongea yenyewe kuwa wawili hao ni kapo (wapenzi).

 

Ulifika wakati, Ijumaa Wikienda lilimvaa Linah na kutaka kujua kinachoendelea kati yake na jamaa huyo kwani minpng’ono ilikuwa ni mingi kwa watu waliowaona.

 

Linah alionesha hali ya kupaniki na kugomba huku akilitaka gazeti hili kuacha kumuingilia katika mambo yake binafsi.

 

 

 

“Sitaki mambo ya umbeya, kwa hiyo nisiambatane au kukaa na mtu? Kwanza sioni cha ajabu kwa sababu sasa hivi nipo huru na mambo yangu, naweza kufanya chochote ninachojisikia na hakuna wa kuniwekea mipaka katika uhusiano wala kazi zangu, niacheni na mambo yangu tafadhali,” alisema Linah ambaye analea mtoto mmoja aliyezaa na Mchomvu.

Na Musa Mateja | na Shamuma Awadhi

Serikali Yapania Kutokomeza Unyanyasaji, Yaja Na Mbinu Hii

Comments are closed.