The House of Favourite Newspapers

IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO JESHI LA POLISI – VIDEO

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amembadilisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kabla ya kuhamishiwa Makao Makuu ya Polisi, DCP Ahmed Msangi kuwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na Msemaji wa Jeshi hilo akichukua nafasi ya ACP Barnabas Mwakalukwa ambaye ameteuliwa kuwa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Pwani.

 

Aidha, Jeshi la Polisi nchini limewataka wananchi wote kutii Sheria bila shuruti katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka na kusema hakuna atakayekuwa salama endapo atavunja sheria za nchi.

 

Msangi amewatahadharisha waganga wa kienyeji wanaotumia Ramli chonganishi kuacha mara moja kwa kua tayari makamanda wote wa Jeshi hilo hapa nchini wameshapewa maelekezo kuhusiana na watu hao ambao wanakwenda kinyume cha Sheria.

 

“Siku chache zilizopita kuna watu ambao wamekuwa wanajikusanya na kufanya uhalifu kwa kutumia silaha, sasa nataka niwaambie acheni mara moja mkipatikana hatutakua na huruma,” amesema Msangi.

 

Ameongeza kuwa Takwimu za Makosa ya Jinai zimetajwa kupungua kutoka 496,677 kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba ya mwaka 2017 na mwezi Januari hadi Oktoba 489429 ya mwaka 2018 ,ambayo inatajwa kua ni pungufu ya makosa 7248 sawa na 1.5%.

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.