The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Majimaji Yafanya Kweli, Yaivuruga Stand United

0
Wachezaji wa timu ya Majimaji wakishangilia kwa pamoja.

Kikosi cha Majimaji cha mkoani Ruvuma mjini Songea kimefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya Vodacom kutokana na kuifunga Stand United bao 1-0.

 

Ushindi huo umepatikana leo Ijumaa katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea ambapo ulihudhuriwa na mashabiki wachache, hali ambayo inadaiwa ilitokana na Majimaji kutofanya vizuri katika michezo yake ya mwanzoni.

Majimaji ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya Sokabet inayojihusisha na kubashiri matokeo, ilianza mchezo huo kwa kasi ndogo lakini kadiri muda ulivyosonga ndivyo ambavyo kasi iliongezeka.

 

Hadi kipindi cha kwanza kinakamilika matokeo yalikuwa 0-0, kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa wenyeji kuonyesha uwezo wa kuvutia na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa mshambuliaji Marcel Boniventure.

 

Boniventure alifunga bao hilo likiwa ni bao lake la tatu katika ligi kuu msimu huu wa 2017/18, hivyo kutokana na matokeo hayo sasa Majimaji imefikisha pointi 8 katika michezo tisa, baada ya kushinda mmoja, sare tano na kupoteza michezo mitatu.

 

Ikumbukwe kuwa vinara wa ligi hiyo ni Simba wenye pointi 16 sawa na Yanga na Azam FC, huku wanaoshika mkia ni Ruvu Shooting wakiwa na pointi tano.

 

Leave A Reply