The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Tecno Camon 16s Yazinduliwa Rasmi

0
Msanii wa bongo Muvi Elizabeth Michael (LULU) akipiga selfie kwa TECNO CAMON 16s

Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imezindua rasmi  simu yake mpya toleo la CAMON 16s leo jijiini Dar es Salaam pamoja na kuwatambulisha mabalozi wa simu hiyo.

 

 Akizungumza  wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, meneja mahusiano wa kampuni hiyo bwana Eric Mkomoya amesema simu hiyo sio tu imelenga kurahisisha mawasiliano bali kuleta mapinduzi katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinazotegemea zaidi  teknolojia hasa upande wa kamera.

 

“Pamoja na kwamba simu ni kifaa cha mawasiliano lakini kutokana na sifa za TECNO CAMON 16s mtumiaji akiitumia kwa ufanisi itampa maslahi makubwa kuanzia wafanyabiashara, wajasiriamali , wasanii,  wafanyakazi maofisini na hata wanafunzi wa vyuo vikuu” Amesema Mkomoye.

 

Mtangazaji Omary Tambwe katika pozi akipiga selfie kwa ktumia TECNO CAMON 16s

 

Akibainisha baadhi ya sifa za simu hiyo Mkomoye amesema TECNO CAMON 16s ina kioo kikubwa chenye inchi 6.6, kamera nne nyuma na huku kamera kuu ikiwa na 48MP, amesema ukubwa wa kamera hiyo unaiwezesha Camon 16s kuchukua picha ang’avu bila kujalisha mazingira au muda ambao picha inapigwa hata kwenye mwanga hafifu ikiwezeshwa na flashi zake nne za nyuma pamoja na lensi yenye teknolojia ya AI.

Mwonekano wa mbele na nyuma wa TECNO CAMON 16s   

                               

                            

 

“Pamoaja na kuwa na kamera kubwa yenye uwezo, pia simu TECNO CAMON 16s ina memori kubwa inayofikia GB 128 ROM kwa GB 4 RAM. Ukubwa wa memori ya simu hii utamsaidia mtumiaji kuhifadhi vitu vyake bila kufuta pia kuiwezesha simu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi bila kukwamakwama” Aliongeza Mkomoye.

                        

Mlimbwende Jihan Dimack na Muigizaji Lulu wakitazama selfie zilizopigwa na TECNO CAMON 16s.

 

Akiwatambulisha mabalozi wa TECNO CAMON 16s, Mkomoye alisema  mabalozi hao watashirikiana na kampuni hiyo ili kurahisisha kufikisha ujumbe kwa  wateja na watu wote wanaopenda kutumia simu zenye teknolojia ya kisasa. Mabalozi hao ni pamoja na  Omary Tambwe,  Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye ni msanii wa bongo muvi pamoja na Miss University Bi. Jihan Dimack.

Kufahamu zaidi ujio wa simu hii bofya link kwenda kwenye ukurasa wao wa Instagram; https://cutt.ly/VgDoVDQ

Leave A Reply