The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Wafugaji Wakubali Kuzika Ndugu Zao Waliopigwa Risasi na Polisi, Bagamoyo

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akiwasili kijijini hapo.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba leo Machi 7, 2017 alifanya kikao cha upatanishi na wafugaji wa jamii ya Kibarbaig ambao waligomea kuzika miili ya vijana wawili ambao ni ndugu wa familia moja, Rumai Kambererega (22) na Sainga Kambererega (25).

 

Mwigulu akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Wafugaji Tanzania, George Bajuta.

Vijana hao wanadaiwa kupigwa risasi na polisi, Jumanne iliyopita katika oparesheni ya kuwaondoa wafugaji kwenye Kijiji cha Kidomole Kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo.

Wananchi hao waligoma kuzika miili ya ndugu hao kwa madai kuwa wamekuwa wakionewa na jeshi la polisi hivyo kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba afike kijijini hapo kuzungumza nao ndipo wanaweza kukubali kuzika.

Mbali na hayo, jana ilikuwa imepangwa wazike lakini waligoma kufanya hivyo na hata alipokwenda Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo waligoma pia kumsikiliza.

Wafugaji hao walikuwa wakilaani kitendo kilichofanywa na polisi hao ambapo walidai mwaka jana walimuua mfugaji mwingine aliyeitwa Gegona Moram na wauaji hawakuchukuliwa hatua yeyote.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Waziri Mwigulu Nchemba wakiwasiliza wanakijiji hao

Katika kikao hicho muafaka uliweza kupatikana ambapo wafugaji hao walikubaliana na kuizika miili ya ndugu zao kesho.

Mwenyekiti wa Wafugaji akizungumza jambo.

Usikose Makala Maalum kuhusu sakata hilo! Ni Jumatano hii Februari 7, 2017. YouTube Channel ya GLOBAL TV ONLINE.

Baba wa marehemu, Kamberega.

Mama wa Kibarbaig akitoa ya moyoni juu ya uonevu wanaofanyiwa na polisi

PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS NA ISAA MNALLY | GLOBAL PUBLISHERS.

Comments are closed.