The House of Favourite Newspapers

HAWA NDIYO MAQUEEN WA…BEN 10 NIZATION!

Tokeo la picha la uwoya na dogo janja

MOJA kati ya vitu vilivyozoeleka kwenye jamii zetu katika masuala ya uhusiano kati ya mwanaume na mwanamke ni umri.Tumezoea siku zote kuwa ni lazima mwanamke awe na umri mdogo kuliko mwanaume, yaani mwanaume lazima awe na umri mkubwa. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia na ujio wa Wazungu, basi hilo limebadilika, hivi sasa unaambiwa umri siyo kitu, bali ni namba tu, cha maana ni mapenzi ambayo haijalishi una umri gani. Ben 10 ni katuni maarufu inayopendwa na watoto. Katuni hii imekuwa ikifananishwa na wanawake wanaopenda na kukithiri kwa kupenda vijana wadogo.

Huu unatajwa kuwa ugonjwa mpya wa mastaa wa kike nchini ambapo uchunguzi wangu unaonesha kuwa kati ya wanawake kumi, basi watano wanafurahia kushiriki tendo la ndoa na vijana hao wadogo. Tabia hii imeibua jina la Kingereza lisilo rasmi la Ben10nization! Ukweli ni kwamba, ishu hii inaonekana kuwavutia wengi kuanzia watu wa kawaida, mashuhuri, mastaa na viongozi mbalimbali. Lakini wengi wamekuwa wakijiuliza, kwa nini baadhi ya wanawake hao wanavutiwa na viben 10 Uchunguzi wangu umebaini kwamba, kuna sababu kadha wa kadha zinazochochea jambo hilo;

Mosi; Kuna nadharia kuwa, binadamu hupenda kutenda jambo linalokatazwa kwenye jamii ili kuona itakuwaje? Wanawake ambao umri umekwenda hukatazwa kuwa na kijana mdogo ili kutunza utamaduni wa Kiafrika na kujitunzia heshima ikiaminika kuwa akiwa na kijana mdogo atapoteza heshima ya kuwa chini ya utawala wa mwanaume aliyemzidi au kulingana naye kiumri na kupokea maelekezo ya utii, jambo ambalo linaaminika vijana wadogo hutawaliwa na mwanamke hivyo kushindwa kumpa maelekezo na maonyo kama mume.

Pili; Sababu nyingine, baadhi ya wanawake hushawishiwa na wenzao kwa kuaminishwa kuwa vijana wadogo bado wana maziwa ya mama zao tumboni hivyo linapokuja suala la ufanisi wa tendo la ndoa, basi hufanya vizuri zaidi na kuwamalizia ‘shida’ zao za kimapenzi.

Tatu; Lipo suala la kasumba ya baadhi ya wanawake ambao huamini kuwa akiwa na kijana mdogo, basi ni rahisi mno kumtawala tofauti na watu wazima wenzao.

Hizo ni baadhi ya sababu ambazo zinatajwa zaidi, lakini kwenye ulimwengu wa wasanii wa sinema na muziki nchini, wapo baadhi ya mastaa wa kike (maqueen) ambao wapo au walishakuwa kwenye mapenzi katika ndoa au uhusiano kama ifuatavyo;

UWOYA KWA DOGO JANJA

Katika mahojiano mbalimbali, Irene Uwoya ambaye ni staa wa sinema za Kibongo aliyezaliwa mwaka 1988, mara kadhaa amekuwa akikiri kwamba, mpenzi au mumewe, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ aliyezaliwa mwaka 1994 ni kibenten wake kwani jamaa huyo wa Bongo Fleva ni sawa na mdogo wake, japokuwa anamkubali mno kutokana na namna anavyommalizia haja zake za kimapenzi.

SHILOLE KWA UCHEBE

Achana na taarifa za huko nyuma kwamba alisharuka kimapenzi na dogodogo wengi aliowazidi umri, lakini kwa sasa yupo kwenye ndoa na Sharrif Uchebe ambaye amempita umri ile mbaya.

RIYAMA KWA LEO

Achana na hao, kuna mkongwe mwingine wa sinema za Kibongo, mwanamama Riyama Ally ambaye alianza kidogokidogo na msanii wa Bongo Fleva, Leo Mysterio kabla ya kufunga naye pingu za maisha huku Riyama akikiri kumpita umri mwanaume huyo.Tokeo la picha la wolper na brown

WOLPER KWA BROWN

Jacqueline Wolper alishatajwa na wanaume wengi lakini ambaye alikiri kumpia umri ni staa wa Bongo Fleva, Harmonize na mwanamitindo Brown.

NISHA KWA MINU

Kabla ya kuingia kwenye mgogoro mzito na kunyang’anywa mwandani wake, Minu Calypton na staa wa muziki Bongo, Snura Mushi, Nisha alishaweka wazi kuwa kwenye mapenzi na jamaa hiyo ilihali akijua kabisa ni sawa na mdogo wake.Picha inayohusiana

AUNT KWA MOZE IYOBO

Naye mwigizaji wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel mwenye umri wa zaidi ya miaka 30, yupo kwenye mapenzi motomoto na Moze Iyobo, mwenye umri wa chini ya miaka 23, ambaye ni mnenguaji wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Picha inayohusiana

SNURA KWA MINU CALYPTO

Baada ya kumpora kwa staa mwenzake, Salma Jabu ‘Nisha’, Snura Mushi naye alianza kutamba kuwa Minu ni kibenten wake na wala suala umri halimnyimi usingizi.

SISTER FAY KWA HOLY STAR

Hivi karibuni msanii wa Bongo Fleva, Faiza Omary ‘Sister Fay’ alifunguka namna anavyomzimia kibenten wake, Holy Star ambaye anampa raha zote za dunia hivy hahitaji mtu mzima mwenzake.Tokeo la picha la wema sepetu and idris sultan

WEMA KWA IDRISS

Wema Isaac Sepetu aliyezaliwa mwaka 1988 aliwahi kuwa kwenye mapenzi na Idriss. Hata kipindi kifupi cha kuwa pamoja, Wema aliweka wazi kuwa Idriss aliyezaliwa mwaka 1993 ni kweli alikuwa sawa na mdogo wake.

ZARI KWA DIAMOND

Kwa upande wake Zari ambaye ni mzazi mwenza wa Diamond anatajwa kuwa na umri mkubwa kuliko jamaa huyo. Inafahamika kwamba, Zari alizaliwa mwaka 1980 wakati Diamond aliliona jua mwaka 1989.

 

Comments are closed.