The House of Favourite Newspapers

Hazard: Messi Ndiye Mchezaji Bora Wa Dunia

Lionel Messi wa Barcelona.

STAA wa Chel­sea, Eden Hazard amesema kuwa kwake yeye Lionel Messi wa Barcelona ndiye mchezaji bora wa dunia.

Kauli hiyo ya Hazard im­ekuja ikiwa ni wiki chache kabla ya Chelsea kukutana na Barcelona katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, pia ikiwa inamaanisha kuwa Messi ni zaidi ya Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambaye ndiye mpinzani wake mkuu.

“Unapocheza soka lazi­ma ufurahi kucheza dhidi ya wachezaji bora na timu bora. Messi ni mchezaji bora wa dunia,” alisema Hazard.

Comments are closed.