The House of Favourite Newspapers

HEAVY DUTY RANGES: JIKO LINALOTUMIA UMEME NA GESI KWA PAMOJA – VIDEO

UKIWAULIZA watu wengi, kama wamewahi kuona jiko la gesi, bila shaka jibu litakuwa ni ndiyo. Ukiwauliza pia watu wengi kama wamewahi kuona jiko la umeme, pia majibu mengi yatakuwa ni ndiyo.  

 

Lakini ukiwauliza watu haohao, je, umewahi kuona jiko linalotumia umeme na gesi kwa wakati mmoja? Utaona jinsi majibu ya ndiyo ya­takavyopungua au kukosekana kabisa.

Hii ni kwa sababu ni teknolojia mpya kabisa hasa katika nchi za ulimwengu wa tatu. Basi kwa taarifa yako, na wewe unayo nafasi ya kumi­liki jiko la aina hii kwa bei poa kabisa. Hii ni miongoni mwa bidhaa nyingi zinazopatikana katika maduka ya Uni Industries yaliyopo jijini Dar es Salaam na Zanzibar na kusambaa kwenye nchi za Kenya, Uganda na Rwanda.

 

Uzuri wa jiko hili ni kwamba lina uwezo wa kuivisha chakula kingi ndani ya muda mfupi, huku likiwa limetengenezwa kukidhi mahitaji ya wapishi kuanzia wa majumbani, mpaka mahotelini. Umeme ukika­tika kama ulikua unapika, unabadili mfumo tu na kuendelea kupikia gesi, pia gesi ikiisha ukiwa unapika, una­badilisha mfumo na kutumia umeme.

Kwa jinsi lilivyotengenezwa, lina­tumia umeme kidogo huku likitoa nisha­ti ya kutosha, lakini pia ukibadili­shana kuanza kutumia gesi, kiwango kinachotumika ni kido­go kulinganisha na moto unaotoka. Muundo wake unafanya iwe rahisi kulisafisha baada ya kupika, na ina droo maalum unazoweza kuzitumia kuhifadhia chakula kisiharibike kwa muda mrefu.

 

Mbali na jiko hili la kisasa, pia Uni Industries wana bidhaa nyingine, likiwemo jiko la kisasa la Atolspeed Hybrid Oven, lenye uwezo wa kuoka mikate kwa wingi na ndani ya muda mfupi, mara tatu zaidi ya majiko ya kawaida ya kupikia mi­kate, huku likitumia nishati kidogo.

“Tunavyo vifaa vingi kwa ajili ya mahitaji kuanzia ya jikoni, mahotel­ini, supermarket na mashine za ku­fulia. Bidhaa zetu zina kiwango cha kimataifa na mteja anaponunua, anakuwa na uhakika wa fedha zake kwa kipindi kirefu,” alisema Roscoe Bremer, Meneja wa Kanda wa Uni Industries.

 

Kwa mahitaji ya vifaa vingine vingi vya kisasa, tembelea maduka ya Uni Industries yaliyopo Staywell Com­plex, plot 1720, Haile Sellasie Road, mkabala na Marrybrown, Namanga jijini Dar es Salaam na Forodhani, Zanzibar.

 

Bidhaa nyingine zinazopatikana Uni Industries ni pamoja na vifaa mbalim­bali kwa matumizi ya jikoni kama vile mashine za kisasa za kuoka vyakula, kupikia keki, kukata mbogamboga na matunda, kutengenezea juisi na kadhalika.

Lakini pia wanauza vifaa vingine kama majokofu ya kisasa ya uku­bwa tofautitofauti, vifaa vya kusam­bazia vyaku­la kwenye sherehe na shughuli mbalim­bali (catering services), mashine za kufulia, vifaa vya supermarket kama ‘shelves’ za kisasa, vitoroli vya kube­bea bidhaa supermarket, samani za ndani na vingine vingi.

 

Pia unaweza kuwasiliana nao kwa simu namba 0681 111 999 au 0766 075 031 au kwa barua pepe [email protected]. Pia unaweza kutembea website yao kwa kubofya www.uni-eastafrica.com. Wahi sasa ili uwe miongoni mwa watu wanaok­wenda na wakati kwa kumiliki vifaa vya kisasa vyenye teknolojia ya hali ya juu.

 

Mwenye Maduka Haya Bongo, Kamgusa Magufuli Penyewe!

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.