The House of Favourite Newspapers

LOWASSA AUNGANA NA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA RUGE

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa leo asubuhi wamefika nyumbani kwa Prof. Mutahaba ambaye ni baba mzazi wa Ruge Mutahaba aliyekuwa mkurugenzi wa uzalishaji vipindi wa Clouds Media Group kutoa pole na kuwafariji wafiwa.

Mwili wa Ruge Mutahaba unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam kutokea Afrika Kusini siku ya kesho IJUMAA, Machi 1, 2019.

Wakazi wa Dar es Salaam watatoa heshima za mwisho na kumuaga mpendwa wetu siku ya JUMAMOSI, Machi 2.

Baada ya hapo: Familia imeamua kwamba Ruge atakwenda kuzikwa nyumbani kwao huko Bukoba,  hivyo mwili utasafirishwa kwenda Bukoba Jumapili na siku ya JUMATATU, Machi 4, 2019 utapumzishwa katika nyumba yake ya milele.

Comments are closed.